UPENDO NI NINI?
Upendo umetokana na neno la kigiriki “ahab
aheb” lenye maana hisia kali na
muhathirika wa ndani.
Upendo ni hisia kali, upendo chimbuko lake ni moyoni
upendo ni Mungu ameuweka ndani ya moyo
wa mwanadamu, upendo ni maisha
ya mtu na ni utaratibu wa mtu hivyo mtu anapo amua kumpenda
mtu mwingine mtu huyu anakua ameamua
kuhatarisha maisha yake kwa mtu Fulani.
Ameamua kuuweka
moyo wake kwa mtu Fulani. Ameathirika ndani ya moyo wake kwa
ajili ya mtu Fulani akili ambayo ndio
chanzo cha mapenzi imekubaliana nayo.
Najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni akili,kama akili ikichoka hakuna
mapenzi
hivyo ndio maana hata maandiko yanasema “ Ishini
na wake zenu kwa akili”
Maana mapenzi la kweli yanahitaji akili
timamu uwe na muda wa kufikiri kabla ujafanya lolote. Kuishi na mtu
kunahitaji
akili timamu, sasa mtu huyu amefanya maamuzi ya kiakili, kimwili na kiroho kuwa wewe unamfaa
hivyo unatakiwa kuyaheshimu na kuyadhamini mawazo yake na kuyatendea
kazi kwa uangalifu sana
UPENDO NI MSUKUMO WA NDANI YA MTU.
Upendo si kitu cha kuchezea mpendwa
mwenzangu. Upendo ni uhai wa mtu.
Ndiyo maana maandiko yanasema: “Upendo una nguvu kuliko mauti”
Hili andiko wewe unalielewaje? Mimi ninavyolielewa ni kuwa
Upendo ni zaidi ya kifo yaani Upendo ni
heri
kuchagua kifo kuliko kuchagua kupenda au kupendwa maana upendo umekamata moyo na wewe
unaelewa kazi ya moyo
kwa mtu? HEART – kwa kiyunani ni (leb) – mind
ni ufahamu,
midst (labab) Kiyunani –
inner person – yenye maana ya undani wa mtu – mind and heart – which also
includes decision making ability- (ufahamu na moyo ambayo hujumuishwa pia maamuzi
yanaweza kufanyika (Mwanzo 6:5-6) vilevile
moyo unasimama kama (kiungo cha mwili) 2Sam
18:14- can be used of the innerman- undani wa mtu unaweza kutumika hivyo.
Moyo unakuwa kama – hisia (emotions Kumb 6:5) moyo – furaha waamuzi
16:25
Moyo una hofu na huzuni ISam
24:10
Moyo unaweza kujaribiwa zab
86:11
Hivyo maumivu ya moyo sio mchezo, haya ni maumivu ya ndani kwa
ndani. Maumivu yake yanatembea ndani ya damu haya ni mateso makubwa sana maana
unaweza ukawa umelala mwili lakini nafsi hailali inahangaika usiku kucha –
unauwezo mkubwa wa kwenda kulaa umechaka na kuamka umechoka maana nafsi ilikuwa
inatafuta.
a)
kufarijiwa
kutiwa moyo,
b)
upendo
kudhaminiwa,
c)
kuheshimiwa,
d)
kukubalika,
e)
kutambulika
na mtu anayefaa maana upendo hautafuti watu bali unatafuta mtu haijalishi awe
amesoma, hajasoma, tajiri au masikini, mweupe au mweusi, mfupi ama mrefu Upendo
unamtafuta mtu (a person)
Moyo – ndio eneo ambalo maamuzi yenye nguvu
yanafanyika – kuaminiana ndio maana hata maandiko Matakatifu yanasema “Mtu moyoni huamini na kwa kinywa hukiri na
kupata wokovu” na andiko lingine linasema
“Watu hawa wananiheshimu
kwa midomo tu lakini mioyoni mwao wako mbali nami”
Hivyo upendo wa kweli huanzia moyoni. Unaamini tokea moyoni kuwa
huyu ndiyo, anayenifaa katika moyo wangu, unamdhamisha tokea moyoni mwako
anakuwa na kibari kikubwa maishani mwako kuwa huyu ndiye kisha kwa kinywa
unamdhibitisha kuwa ndiye.
Inaeendelea...
No comments:
Post a Comment