Friday, 4 October 2013

JE UNAJUA AINA ZA MAPENZI NI NGAPI ?



1.    Philotheos                 -        upendo wa mungu; 2timoth 3:4

2.    Philoxenos                -        kupenda wageni [ xenia…..hospitality
3.    Philagathos               -        kupenda kitu kizuri; titus 1:8
4.    Philarguros               -        kupenda pesa; luke 16:14 and 2timoth 3:2
5. Philautos                   -        kumpenda mtu mmoja; 2timoth 3:2
6.  Philedonos                -        kupenda starehe; 2timoth 3:4

Unajua ni vizuri sana kama utapenda mahali unapopendwa kuliko kupenda mahali usipopendwa, unatakiwa uwe na ufahamu mkubwa sana wa mapenzi kabla ya kuyaingia unaweza kupoteza ndoto zako za maisha, maaana mapenzi yanauwezo mkubwa sana wa kuharibu maisha yako. Mabinti wengi na vijana wamejikuta wameingia katika mchezo huu wa mapenzi wakiwa na akili za kitoto huku wakijua kuwa upendo ni kitu cha kawaida leo wanalia sana kutokana na maumivu waliyoyapata. Rafiki yangu ningependa nikwambie Upendo ni nini ?


1.    Upendo ni mzuri sana kama utajua maana na kusudi la Mungu kuweka pendo ndani ya mtu.
2.    Upendo unatesa
3.    Upendo unaua
4.    Upendo unakondesha
5.    Upendo unaharibu maisha
6.    Upendo unaharibu utaratibu wa mtu
7.    Upendo unanyonga  maisha
8.    Upendo unaathiri akili ya mtu
9.    Upendo ni gharama
10.Upendo ni shule
11.Upendo ni maisha ya mtu.

Mpendwa wangu neno hili (Upendo) sio kitu cha mchezo, wewe unaweza kuwa ni mtoto, mwanafunzi  hujajipanga bado utaratibu wako wa maisha unatakiwa uwe makini sana katika jambo hili, unajua kuwa Upendo unauwezo mkubwa sana wa kutoa ufahamu wa mtu na kuharibu utaratibu wa mtu? Upendo unapoingia ndani ya moyo mtu anauwezo mkubwa wa kukutoa  katika mipango yako, upendo ukikolea watu wanauwezo wa kusahau familia zao, masomo, kazi zao, na utaratibu wake wa kila siku unaharibika,  upendo unatakiwa kuheshimika na kila mtu unatakiwa kutembea katika upendo kwa unyenyekevu mkubwa, utiifu na adabu maana sio jambo la mchezo, usichukulie  jambo hili kitoto unatakiwa unapoamua kufanya maamuzi ya kupenda au kupendwa unatakiwa uwe na maswali (14) hayo ya msingi ili usije kuumia kama sisi tulivyoumiza na kuumizwa bila kujua, maana yake na gharama yake.

Itaendelea...

PENZI LA KWELI LINAONGEA MOYONI.


PENZI LA KWELI LINAONGEA MOYONI


1.    Moyo huthibitisha kuwa huyu ndio anayenifaa maishani mwangu.
2.    Aliyepata kibali moyoni mwangu.
3.    Ndiye niliyemtafuta usiku na mchana.
4.    Aliyeutesa moyo wangu.
5.    Aliyeuyumbisha moyo wangu mara tu nilipomwaona.
6.    Mwenye uwezo wa kutimiliza ndoto yangu.
7.    Kioo cha maisha yangu.
8.    Faraja wa moyo wangu.
9.    Huyu ndiyo mwandani wangu (msiri)
10.Kitambulisho cha maisha yangu.
11.Mbeba maono yangu.
12.Heshima yangu katika jamii itakayo nizunguka.
13.Mtetezi wangu asiyeweza kuvumilia nisipate aibu katika jamii.
14.Mfuta machozi na majasho yangu.
15.Mratibu wa moyo wangu.
16.Chemichemi ya furaha yangu.
17.Barafu wa moyo wangu.
18.Asali wa moyo wangu.
19.Malkia na Mfalme wa moyo wangu.
20.Chanzo cha afya yangu.
21.Mjenzi wa familia yangu.
22.Mwalimu wa familia yangu.
23.Mlinzi wa ndoto na maono yangu.
24.Adui wa adui zangu.
25.Mponyaji wa majeraha yangu yaani doctor wa moyo wangu.
26.Rafiki wa moyo wangu.
27.Ngao ya moyo wangu.
28.Ufunguo wa maisha yangu.
29.Ua la moyo wangu.

Huyu ndiye mpenzi anayetafutwa na mtu yoyote katika Dunia hii ya leo mwenye sifa hizi mpendwa, mapenzi yana nguvu sana kuliko unavyodhania kuna watu walikosea katika kuchagua leo wanalia usiku na mchana ndoa imekuwa ndoano mapenzi yamevamiwa na shubiri, moto umewaka matusi, dharau, kiburi, jeuri, ngumi ndio yamechukua maisha kweli mapenzi yanatesa moyo, yanaumiza, yana katisha tamaa, yana poteza maana ya mtu, yanavuta mauti ukiyakosea utanielewa ninamaanisha nini? –MOYO ndio chanzo cha furaha – ukichafuliwa furaha hukimbia na amani, hapo ndipo hofu inapochukua nafasi unajikuta unaanza  kumuogopa mpenzi wako, na wakati upendo wa kweli hauna hofu hata kama mke au mume ni mkali namna gani Upendo wa kweli huondoa hofu lakini ukiona mtu anamuogopa mwenzi wake hapo tambuakuwa penzi hilo limevamiwa na adui, moyo umepoteza dira umekosa matumaini na huyo uliyenaye, Hofu huvuta dhambi hapo ndipo unapoweza kuona mtu anatafuta rafiki mwingine ili aweze kumlinda kumrudishia amani yake, kumponya majeraha yake hapo sio mchezo inabidi unapotambua hivyo unatakiwa kutengeneza maana hapo ndio chanzo cha magonjwa, talaka n.k fanya kwa bidii kujiaminisha katika moyo wa mwenzi wako ili mambo yasiharibike  
Moyo ukiumizwa HUZUNI hutokea hapo ndipo maombolezo yanapoanza, mtu huyu utamkuta analia kila unapomuona na machozi yanamdondoka,

[a]   moyo wake unalia.
[b]   Moyo wake unatoa damu kidonda kibichi.
[c]   Maombolezoyaliyo beba majuto kwa nini nilikubali kuwa na huyu?
[d]   Kama ningelijua nisingekubali.
[e]   Alitokea wapi huyu, Ee Mungu mbona ulimruhusu huyu mtu kuchukua moyo wangu najuta kukutana naye
[F] Amepoteza furaha ya moyo wangu, ameharibu udhamani wa maisha yangu, msambaratishaji wa ndoto yangu.
[g] Adui wa maisha yangu mpinzani wa maendeleo yangu.

Haya maombolezo yanapozidi kuendelea mtu huyu anaamua kufanya maamuzi ambayo wengi hawataweza kukubaliana nayo,  ila yupo kwenye harakati ya kujiokoa nafsi yake hata kufikia kuchukia kupenda au kupendwa maana teso alilopata ni kubwa sana wewe usifanye unajua sana kuongea hujui teso la mapenzi hujui moyo wa mtu ulivyoumizwa – usidanganyike na muonekano wake – aliyeumia yupo.
Unaweza kumuona amelala kitandani na wakati mtu wa ndani amekaa kwenye mkeka anamsiba mkubwa,

[a]   Machozi hayamuishi
[b]   Mawazo yamemsonga sana,
]c]   Moyo umesafiri haupo pale,
[d]   Kazi haziendi,
[e]   Huduma yake inazidi kuharibika kila siku,
[f]    Afya inakwisha kila siku,
[g] Ofisini haonekani kazini anakuja lakini nafsi yake haipo pale na hata wengine wanaweza kutambua kuwa mwenzetu hayupo hapa.
 Unaweza kuongea na mtu ambaye nafsi yake ipo nyumbani kwake sio mchezo. Hapo ndio chanzo cha Msongo wa mawazo hutokea, moyo ulioumizwa kimapenzi unahitaji uangalifu sana kuutibu na kuushauri. Wachungaji wengi wamechangia ndoa za wengi kuvunjika kwa kutokuwa na ufahamu mkubwa wa upendo na matokeo yake, usiwe mwepesi wa kutoa maandiko mengi wakati hujui mateso ya mapenzi najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni sumu, yanapoharibika hutakiwi kuwa mwepesi kuyaingilia maana mapenzi yamebeba maisha ya mtu,
Unapotaka kumshauri mtu aliyeathirika na mapenzi unatakiwa kuyafahamu mambo haya muhimu nayo ni:-

1.    Unatakiwa kujua maana ya upendo na gharama zake.
2.    Lazima ujue vyanzo vya kujenga uhusiano ili uwe imara na mwenye   nguvu katika maisha ya wapendanao.  
3.    Mambo 32 yanayojenga uhusiano kama ulivyosoma.
4.    Lazimaujue mambo yanayoweza kuharibu mahusiano na milango ya kuvunja mahusiano.
5.    Lazima ujue maumivu ya mapenzi ili uweze kuwaponya waliojeruhika kimapenzi.

Nina maswali ya kujiuliza kuhusu UPENDO jambo hili ni kubwa sana katika maisha ya mwanadamu hakuna asiyejua maana limechukua sehemu kubwa katika MOYO wa mwanadamu,watu wengi tumekuwa tunalia sana, tumekuwa tunakata tamaa,tumekuwa tukigombana, hata hatua ya kuumizana na wengi wamekufa na wengi hawataki kupenda tena. Na kundi lingine linasema kupenda ni mzuri  sana wanasema unanguvu sana na wakati mwingine wanasema kupenda ni kifo na wanaona unakupeleka jehanamu katika sehemu saba zifuatazo:

1.    Sehemu ya mateso
2.    Sehemu ya mahangaiko
3.    Sehemu ya masikitiko
4.    Sehemu ya magomvi
5.    Sehemu ya matukano
6.    Sehemu ya kudhalilishwa
7.    Sehemu ya kuchafuliwa

Kwa nini tunapenda na kwa nini tunatumia ikiwa upendo ni mzuri Ni nani anayesababisha nipende na ninanianyenipenda kweli? Ni ninani nitayempenda? Na kwanini upendu unanguvu na imechukua sehemu kubwa ya maisha yangu? Sasa upendo ni nini na inamaana gani?

UPENDO NINI?


UPENDO NI NINI?
 Upendo  umetokana na neno la  kigiriki “ahab aheblenye maana hisia kali na muhathirika wa ndani
Upendo ni hisia kali, upendo chimbuko lake ni moyoni upendo ni Mungu  ameuweka  ndani ya moyo 
wa mwanadamu, upendo ni maisha ya mtu na ni utaratibu wa mtu hivyo mtu anapo amua  kumpenda 
mtu mwingine mtu huyu anakua ameamua kuhatarisha maisha yake  kwa mtu Fulani. Ameamua kuuweka 
moyo wake kwa mtu Fulani. Ameathirika ndani ya moyo wake kwa ajili ya mtu Fulani akili ambayo ndio
 chanzo cha mapenzi imekubaliana nayo. Najua kuwa unajua kuwa mapenzi ni akili,kama akili ikichoka hakuna 
mapenzi hivyo ndio maana hata maandiko yanasema “ Ishini na wake zenu kwa akili”

Maana mapenzi la kweli yanahitaji akili timamu uwe na muda wa kufikiri kabla ujafanya lolote. Kuishi na mtu
 kunahitaji akili timamu, sasa mtu huyu amefanya maamuzi ya  kiakili, kimwili na kiroho kuwa wewe unamfaa
 hivyo unatakiwa kuyaheshimu na kuyadhamini mawazo yake na kuyatendea kazi kwa uangalifu sana
 UPENDO NI MSUKUMO WA NDANI YA MTU.

Upendo si kitu cha kuchezea mpendwa mwenzangu. Upendo ni uhai wa mtu.
 Ndiyo maana maandiko yanasema: “Upendo una nguvu kuliko mauti
Hili andiko wewe unalielewaje? Mimi ninavyolielewa ni kuwa Upendo ni zaidi ya kifo yaani Upendo ni
 heri kuchagua kifo kuliko kuchagua kupenda au kupendwa maana upendo  umekamata moyo na wewe
 unaelewa kazi ya moyo kwa mtu? HEART – kwa kiyunani ni  (leb)  mind ni ufahamu, 
midst (labab) Kiyunani – inner person – yenye maana ya undani wa mtu – mind and heart – which also includes decision making ability- (ufahamu na moyo ambayo hujumuishwa pia maamuzi yanaweza kufanyika (Mwanzo 6:5-6) vilevile moyo unasimama kama (kiungo cha mwili) 2Sam 18:14- can be used of the innerman- undani wa mtu unaweza kutumika hivyo.

Moyo unakuwa kama – hisia (emotions Kumb 6:5) moyo – furaha waamuzi 16:25
Moyo una hofu na huzuni ISam 24:10
Moyo unaweza kujaribiwa zab 86:11

Moyo unaweza ukawa mgumu wakati mwngine kumb 30:6

Hivyo maumivu ya moyo sio mchezo, haya ni maumivu ya ndani kwa ndani. Maumivu yake yanatembea ndani ya damu haya ni mateso makubwa sana maana unaweza ukawa umelala mwili lakini nafsi hailali inahangaika usiku kucha – unauwezo mkubwa wa kwenda kulaa umechaka na kuamka umechoka maana nafsi ilikuwa inatafuta.

a)    kufarijiwa kutiwa moyo,
b)   upendo kudhaminiwa,
c)   kuheshimiwa,
d)   kukubalika,
e)    kutambulika na mtu anayefaa maana upendo hautafuti watu bali unatafuta mtu haijalishi awe amesoma, hajasoma, tajiri au masikini, mweupe au mweusi, mfupi ama mrefu Upendo unamtafuta mtu (a person)

Moyo – ndio eneo ambalo maamuzi yenye nguvu yanafanyika – kuaminiana ndio maana hata maandiko Matakatifu yanasema “Mtu moyoni huamini na kwa kinywa hukiri na kupata wokovu” na andiko lingine linasema
“Watu hawa wananiheshimu kwa midomo tu lakini mioyoni mwao wako mbali nami”

Hivyo upendo wa kweli huanzia moyoni. Unaamini tokea moyoni kuwa huyu ndiyo, anayenifaa katika moyo wangu, unamdhamisha tokea moyoni mwako anakuwa na kibari kikubwa maishani mwako kuwa huyu ndiye kisha kwa kinywa unamdhibitisha kuwa ndiye.

Inaeendelea...