1. Philotheos - upendo wa mungu; 2timoth 3:4
2. Philoxenos - kupenda wageni [ xenia…..hospitality
3. Philagathos - kupenda
kitu kizuri; titus 1:8
4. Philarguros - kupenda
pesa; luke 16:14 and 2timoth 3:2
5.
Philautos - kumpenda mtu mmoja; 2timoth 3:2
6. Philedonos - kupenda starehe; 2timoth 3:4
Unajua ni vizuri sana kama utapenda mahali unapopendwa kuliko
kupenda mahali usipopendwa, unatakiwa uwe na ufahamu mkubwa sana wa mapenzi
kabla ya kuyaingia unaweza kupoteza ndoto zako za maisha, maaana mapenzi
yanauwezo mkubwa sana wa kuharibu maisha yako. Mabinti wengi na vijana
wamejikuta wameingia katika mchezo huu wa mapenzi wakiwa na akili za kitoto
huku wakijua kuwa upendo ni kitu cha kawaida leo wanalia sana kutokana na
maumivu waliyoyapata. Rafiki yangu ningependa nikwambie Upendo ni nini ?
1. Upendo ni mzuri sana kama utajua maana na
kusudi la Mungu kuweka pendo ndani ya mtu.
2. Upendo unatesa
3. Upendo unaua
4. Upendo unakondesha
5. Upendo unaharibu maisha
6. Upendo unaharibu utaratibu wa mtu
7. Upendo unanyonga maisha
8. Upendo unaathiri akili ya mtu
9. Upendo ni gharama
10.Upendo ni shule
11.Upendo ni maisha ya
mtu.
Mpendwa wangu neno hili (Upendo)
sio kitu cha mchezo, wewe unaweza kuwa ni mtoto, mwanafunzi hujajipanga bado utaratibu wako wa maisha
unatakiwa uwe makini sana katika jambo hili, unajua kuwa Upendo unauwezo mkubwa sana wa kutoa ufahamu wa mtu na kuharibu
utaratibu wa mtu? Upendo unapoingia ndani ya moyo mtu anauwezo mkubwa wa
kukutoa katika mipango yako, upendo
ukikolea watu wanauwezo wa kusahau familia zao, masomo, kazi zao, na utaratibu
wake wa kila siku unaharibika, upendo unatakiwa kuheshimika na kila
mtu unatakiwa kutembea katika upendo kwa unyenyekevu mkubwa, utiifu na adabu
maana sio jambo la mchezo, usichukulie
jambo hili kitoto unatakiwa unapoamua kufanya maamuzi ya kupenda au
kupendwa unatakiwa uwe na maswali (14) hayo ya msingi ili usije kuumia kama
sisi tulivyoumiza na kuumizwa bila kujua, maana yake na gharama yake.
Itaendelea...
Itaendelea...